MABARAZA YA WATOTO YAHIMIZWA KUFICHUA VITENDO VYA UKATILI.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Faustine Ndugulile akihojiwa na wanahabari watoto wa mkoa wa Mwanza wakati alipowatembelea Baraza la Watoto la Mkoa wa Mwanza na kuona shughuli wanazofanya wajumbe wa Baraza hilo. Makamu Mwenyekiti Baraza la Watoto la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akisoma risala kwa Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Faustine Ndugulile kuelezea utekelezaji wa kazi za Baraza la Watoto kwa Mkoa wa Mwanza
Mwenyekiti wa Baraza la Watoto la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Bw. Joel Festo akiishukuru Serikali na wadau kawa kuendelea kuwajali watoto kuanzia katika utoaji wa huduma za afya na kutekeleza upatikanaji wa haki zao za msingi ikiwemo haki ya kuishi, kulindwa, kuendelezwa, kushirikishwa na kutobaguliwa.
Naibu Waziri wa
Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Faustine Ndugulile
akimkabidhi Mtunza Hazina wa Baraza la watoto la Mkoa wa Mwnzxa kiasi cha
Shillingi 250,000/= ikiwa ni mchango wake kwa ajili ya ununuzi wa printa kwa
ajili ya shughuli za ofisi za Baraza hilo.
Naibu Waziri wa
Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Faustine Ndugulile akiwa
katika picha ya pamoja na viongozi wa kitaifa wa Baraza la Watoto na Viongozi
na wajumbe wa Baraza la Watoto la Mkoa wa Mwanza, viongozi wa mkoa na wadau wa
watoto mkoani humo mara baada ya kulitembelea Baraza la Watoto la Mkoa wa
Mwanza na kuona shughuli wanazofanya wajumbe wa Baraza hilo.
Picha zote na Kitengo
cha Mawasiliano WAMJW
Na WAMJW- Mwanza
Mabaraza ya Watoto
nchini yamehimizwa kutumia elimu wanayoipata kuibua vitendo vya ukatili wanavyofanyiwa
watoto ili kuondokana na vitendo hivyo.
Hayo yamesemwa na
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Faustine
Ndugulile wakati akizungumza na wajumbe wa Baraza la Watoto la Mkoa wa Mwanza
alipowatembelea na kuona shughuli wanazofanya wajumbe wa Baraza hilo.
Dkt.Ndugulile amesema
kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2017 takribani wanawake na watoto 41,000 walifanyiwa
vitendo vya ukatili wa kijinsia kati yao 13,000 wakiwa ni watoto pekee.
Ameongeza kuwa
vitendo vya ukatili vimeongezeka ukilinganisha na matukio ya vitendo vya
ujambazi nchini ambapo suala hilo halitakiwi kufumbiwa macho na wananchi na
wadau.
Aidha Dkt. Ndugulile
ametoa rai kwa wananchi hasa wazazi na watoto kutomalizana nyumbani endapo
vitatokea vitendo vya ukatili katika familia zao bali kuviripoti katika mamlaka
husika.
Naye Mwenyekiti wa Baraza
la Watoto la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Bw. Joel Festo ameishukuru
Serikali na wadau kawa kuendelea kuwajali watoto kuanzia katika utoaji wa
huduma za afya na kutekeleza upatikanaji wa haki zao za msingi ikiwemo haki ya
kuishi, kulindwa, kuendelezwa, kushirikishwa na kutobaguliwa.
Dkt Ndugulile pia
ametembelea na kujionea shughuli zinazotolewa na Kituo cha utoaji Huduma za
pamoja kwa wahanga wa ukatili wa kijinsia (One Stop Centre) hapo mkoani Mwanza.
Kwa upande wake Kaimu
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Sekou Toure Dkt. Bahati Peter Msaki amesema
kuwa Kituo cha utoaji Huduma kwa wahanga wa ukatili (One Stop Centre) kimekuwa
msaada mkubwa kwa wanajamii kwani wahanga wengi wa vitendo vya ukatili wamekuwa
wakipata huduma kutoka katika kituo hicho.
Post a Comment