Ads

TAKUKURU YAKAMILISHA UPEPELZI KESI YA MALINZI, WENZAKE

Mwambawahabari

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania( Takukuru) wameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa kwa upande wao wamekwisha kamilisha upelelezi katika kesi inayomkabili aliyekuwa rais Shirikisho la Mpira wa Miguu(TFF) Jamali Malinzi na wenzake.


Mbali na Malinzi wengine ni, Katibu Mkuu wa TFF, Mwesigwa Joas Selestine(46) na Mhasibu wa TFF,  Nsiande Isawayo Mwanga(27).


Wakili wa Serikali kutoka Takukuru, Leonard Swai amedai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu,Thomas Simba,leo mahakamani hapo kuwa upelelezi katika shauri hilo kwa Takukuru umeishakamilika na hadi Jumatatu jalada la kesi hiyo litakuwa limekwisha rejeshwa   (DPP).



Awali, Swai alidai mahakamani hapo jalada la kesi hiyo lilipelekwa kwa DPP ambapo alilipitia na kurirejesha Takukuru kwa maelekezo ambapo wamekwisha yafanyia kazi.Kutokana na taarifa hiyo, Hakimu Simba ameahrisha kesi hiyo hadi Februari 8, mwaka huu.


Washtakiwa hao,       walipandishwa kizimbani kwa mara ya kwanza Juni 29, mwaka 2017, wakikabiliwa na mashtaka 28 ya kughushi na kutakatisha fedha dola za Marekani 375,418. 

No comments