Ads

MILIONI 20 ZATUMIKA KATIKA KAMPENI ZA UPANDAJI WA MITI WILAYANI IGUNGA.


Tokeo la picha la picha za upandaji miti

Mwambawahabari
NA TIGANYA VINCENT
RS-TABORA

JUMLA ya shilingi milioni 20 zimetuma katika kampeni ya upandaji miti katika maeneo mbalimbali wilayani Igunga.
Kauli hiyo ilitolewa jana na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga Revocatus Kuuli wakati wa uzinduzi wa upandaji miti kwa wanachuo wa Chuo cha Sayansi za Afya Nkinga uliofanywa na Mkuu wa Mkoa wa Tabora
Alisema kuwa fedha hizo zimetumika katika ununuzi wa miche ya miti, uoteshaji wa miche na zoezi zima la upandaji katika maeneo mbalimbali kwa lengo la kurudisha uoto wa asili.
Kuuli alisema kuwa kutokana na zoezi hilo kutumia fedha za Halmashauri hiyo zinazotokana na vyanzo vyake wataendelea kupambana na watu wote wanaoenesha uharibifu katika mistu, vyanzo vya maji na wanachunga mifugo katika maeneo ambayo hayaruhusiwi kisheria ili kuhakikisha matunda ya fedha hizo yanaonekana.
Akiongea katika nyakati tofauti na Wanachuo wa Ndala, Nkinga na Kitongo, Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri alisema kuwa kundi hilo la wasomi ni kundi muhimu sana katika kampeni zinazoendelea Mkoani humo.
Alisema kuwa kundi hilo haliwezi kubaki kuwa watazamaji katika zoezi la upandaji miti linapaswa kuwa sehemu ya mradi huo unaoendelea maeneo mbalimbali mkoani humo ili nao wabakize alama kama waliwahi kukaa na kupata elimu na hatimaye kushirikia katika utunzaji mazingira.
Mwanri alisema kuwa hatua hiyo itabaki katika kumbukumbu zao binafisi na za Mkoa wa Tabora.
Alisema kuwa ni jukumu la Wakufunzi kuhakikisha kila mwanachuo kama ilivyo katika Shule za Msingi na Sekondari anakuwa na mti mmoja ambao atautunza katika siku zote ambazo yuko masomoni.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Rufaa ya Nkinga Dkt. Yohana Masonda akisoma taarifa ya Chuo cha sayansi za Afya Nkinga alimpongeza Mkuu huyo wa Mkoa kwa uamuzi wake wa kutumia wanachu mbalimbali kupanda miti katika maeneo yao nay ale ya jamii.
Alisema kuwa wao katika kuunga mkono juhudi za Serikali kuu ya ile ya Mkoa katika suala la uhifadhi wa mazingira tayari wameshapanda miti maji 200 na wanatarajia kuongeza mingine 600 ili kuifanya Igunga kuwa ya kijani.

No comments