Ads

KALIUA WAVUKA LENGO LA UPANDAJI MITI KITAIFA KWA KUPANDA MITI MILIONI 1.8 MSIMU HUU.

Mwambawahabari
Tokeo la picha la picha za miti
NA TIGANYA VINCENT
RS-TABORA

JUMLA ya miti milioni 1.8 imepadwa msimu huo wa 2017/18 katika Wilaya ya Kaliua ikiwa ni sehemu ya kampeni ya kuhifadhi mazingira na mistu na hivyo kuvuka lengo la kitaifa la kupanda miche milioni 1.5 kila mwaka.
Idadi hiyo ni sehumu ya miti milioni 2.1 iliyooteshwa na Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua , Kampuni za ununuzi wa tumbaku na Wakala wa Mistu Tanzania(TFS).
Takwimu hizo zimetolewa jana na Katibu Tawala Wilaya ya Kaliua Michael Nyahinga wakati akisoma taarifa ya upandaji miti kwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora.
Alisema kuwa bustani ya Halmashauri iliotesha miche 210,000 na kupanda miti 174,000, wakati Vyama vya Msingi viliotesha miche milioni 2.1 na kufanikiwa kupanda hadi hivi sasa miche milioni 1.6.
Nyahinga aliongeza kuwa Wakala wa Mistu Tanzania (TFS) wilayani humo ilifanikiwa kuotesha miti 36,000 na hatimaye kupanda miti 12,000 na Kikundi cha KIKUMUMI kiliotesha miche 12,000 na kuweza kupanda 6,000.
Alisema kuwa wangeweza kufanya vizuri zaidi laikini baadhi ya wananchi wamekuwa na mwitikio mdogo katika kampeni hiyo na wengine wamedirikia kung'oa miti inayopandwa katika hifadhi ya barabara.
Akizungumza na wanachuo wa Chuo cha Maendeleo Kaliua na Urambo, Mkuu wa Mkua wa Tabora Aggrey Mwanri wakati wa ziara ya kuhamasisha wanachuo nao kushiriki katika zoezi la upandaji miti mbalimbali kama sehemu ya uwekaji wa alama alisema kuwa ni vema wananchi wakatumia mvua zinaendelea kunyesha kuhakikisha wanapanda miti mingi.
Alisema kuwa baada ya kipindi cha mvua kumalizika itakuwa kazi kubwa katika upandaji na hivyo kuwalazimu kutumia gharama kubwa katika kuhakikisha miti inapona.
Mwanri alisema kuwa kila mkazi wa Tabora lazima hakikishe anapanda miti na kuzuia uharibifu katika mistu kwa kuwaondoa au kutoa taarifa kwa viongozi ili watu wanahusika wachukuliwe hatua.
Alisema kuwa haiwezekani wakazi wa Tabora na viongozi wao waone makosa yanafanyika yanayosababisha uharibifu wa mazingira yanafanyika kisha wao wakae kimya.
“Mimi na nyinyi wananchi sie tuko zamu haiwekani kuona mambo yanaharibika kisha tunasema wache liende…ni kazi yetu kuhakikisha tunarekebisha makosa …kwa kupanda miti kwa wingi na kuzuia uharibufu wa mistu na uvamizi wa vyanzo wa maji”alisisitiza Mkuu huyo wa Mkoa.
Mkuu huyo wa Mkoa amemaliza wiki ya tatu ya kampeni ya upandaji miti kwa kutumia wanachuo na hivyo wiki ijayo ni zamu ya vyama vya siasa.

No comments