TAFEYOCO wamuomba Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli akutane na Vijana.
Na Anitha Jonas
mwambawahabariblog
Shirika lisilo la
kiserikali la Tanzania Feminist and Youth Change Organization (TAFEYOCO)
limemuomba Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuanzisha
utaratibu wa kukutana na vijana ili kujadiliana mambo mbalimbali.
Hayo yamesemwa leo na
Mwenyekiti wa Shirika hilo Bw. Elvis Makumbo alipokuwa akizungumza na waandishi
habari jijini Dar es Salaam katika mkutano uliyolenga kumpongeza
Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe
Magufuli kwa kazi nzuri aliyoifanya katika siku mia moja za uongozi wake.
“Vijana kwa sasa
katika taifa ni wengi na ndiyo wenye uwezo wa kuleta maendeleo katika nchi na
nguvu kazi ya Taifa na wanachangamoto nyingi hivyo Mheshimiwa Rais akijaribu kukutana nao nakuwasikiliza matatizo
yao itasaidia kuleta mafanikio katika nchi na kujua nini kifanyike kuleta
maendeleo katika Taifa,” alisema Bw. Makumbo.
Ameleza kuwa,
Mheshimiwa Rais ameonyesha moyo wadhati wa kuwatumikia wananchi kwa
kuwawajibisha watu wote walionekana wakitumia vibaya madaraka yao na kufanya
ubadhirifu wa pesa za umma kinyume na taratibu za kiutumishi wa umma.
Mbali na hayo
Bw.Makumbo amemuomba mheshimiwa Rais kufikiria kuanzisha mfumo au taasisi
itakayohakiki mali za mtumishi wa umma na kuhoji ni namna gani mali hizo
amezipata ili kupunguza wimbi la watumishi wa umma wanao tumia fedha za
serikali vibaya kwa kujinufaisha wenyewe huku wakijiwekea utajiri mkubwa
usiyolingana na kipato chao.
Mwenyekiti huyo
aliendelea kumwomba Mheshimiwa Rais kuzidi kuzingozea nguvu taasisi za Serikali
ili kuzijengea uwezo mkubwa wa kiutendaji mfano wa Taasisi hizo ni TAKUKURU na
nyinginezo zinazosimamia mambo mbalimbali Yenye tija kwa Taifa.
Shirika hilo limesema
Kauli Mbiu ya Mheshimiwa Rais ya Hapa Kazi Tu imeongeza hari kubwa ya utendaji
kwa wananchi kwa kuwahimiza kuwajibika ikiwemo kwa watu wa sekta binafsi na
taasisi za umma.
Post a Comment