Ads

PROFESA MAKAME MBARAWA ATENGUA UTEUZI WA MTENDAJI MKUU WA WAKALA WA UFUNDI NA UMEME (TEMESA).

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Profesa Makame Mbarawa akitoa taarifa ya utenguzi wa uteuzi wa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme.
(Picha na Benedict Liwenga)
 ………………………………………………………………………………………..
Na Benedict Liwenga.
 
WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Profesa
Makame Mbarawa ametengua uteuzi wa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA), Mhandisi Marcellin Benedict Magesa kuanzia Februari 18 mwaka huu.
 
Profesa Mbarawa amechukua hatua hiyo kutokana na kuwepo kwa
sababu mbalimbali zikiwemo, kushindwa kusimamia matengenezo ya magari na
mitambo ya Serikali nchini, kushindwa kusimamia uendeshaji wa matenegenzo ya
vivuko vya Serikali nchini pamoja na kushindwa kusimamia ukusanyaji wa mapato
kupitia vyanzo mbalimbali.
 
‘’Mhandisi Marcellin Benedict Magesa atapangiwa majukumu
mengine wizarani Na hivyo namteua Mhandisi Manase Lomayani Le-Kujan kuwa Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) kuanzia Leo hii ’’, alisema Profesa Mbarawa.
 
Aidha, Profesa Mbarawa amemuagiza Kaimu Mtedaji Mkuu huyo
aliomteua kutekeleza mara moja mambo mbalimbali, ikiwemo kutengeua uteuzi wa Mkurugenzi anayeshughulikia matengenezo ya magari ya Serikali, Mhandisi Prisca Benedict
Mukama na kumpangia majukumu mengine, pia kutengua uteuzi wa Meneja wa Karakana ya Magari ya Serikali (M.T Depot), Mhandisi John Alexander Mushi na kumpangia
majukumu mengine.
 
Kabla ya uteuzi wake, Mhandisi Manase Lomayani Le-Kujan
alikuwa Mkurugenzi wa Idara ya Huduma za Ufundi na Ushauri katika Wakala wa
Ufundi na Umeme (TEMESA).

PROFESA MAKAME MBARAWA ATENGUA UTEUZI WA MTENDAJI MKUU WA WAKALA WA UFUNDI NA UMEME.

mba
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Profesa Makame Mbarawa akitoa taarifa ya utenguzi wa uteuzi wa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme.
 (PICHA NA BENEDICT LIWENGA

No comments