Ads

NEC YAKAMILISHA MAJUKUMU YA UCHAGUZI 2015/16

NaJacquiline Mrisho
 mwambawa habariblog
Mwenyekitiwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu.Mhe .Damian Lubuva (NEC)  amekamilisha uchaguzi wa mwaka 2015 baada yakumaliza kuteua wabunge wanawake watatu wa viti maalumu waliokuwa wamebakia.  

Uteuzihuo umefanywa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC na kutangazwa rasmi leo JijiniDar es salaam na Jaji Mstaafu Lubuva kwenye mkutano na waandishi wa habariuliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa ofisi za tume hiyo.
“Tumeya Taifa ya Uchaguzi imewateua ndugu Ritah Kabati na Oliver Semuguruka wa Chamacha Mapinduzi (CCM) na Lucy Owenya wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)kuwa wabunge wanawake wa viti maalum katika Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.”alisemaLubuva.


JajiMstaafu Mhe. Lubuva ameongeza kuwa,kwa mwaka 2015 NEC ilitakiwa kuteua wabunge wanawakewa viti maalum 113 ila waliteuliwa jumla ya wabunge 110 ambapo viti vitatuvilibakia kusubiri uchaguzi wa majimbo 8 ambayo uchaguzi wake ulihairishwakutokana na sababu mbalimbali.

JajiMstaafu Lubuva amesema kuwa,NEC hufanya uteuzi wa wabunge wanawake wa vitimaalum kutoka kwenye orodha iliyotumwa na Katibu Mkuu wa chama husika hivyo,Tume imewateua wabunge hao kama walivyoorodheshwa kwenye majina yaliyoletwa namakatibu wao.

Hatimayezoezi la uchaguzi wa mwaka 2015 kwa sehemu zilizosalia  limeisha kwa amani, viongozi waliochaguliwa nakuteuliwa wana wajibu wa kufanya kazi yakuwatumikia wananchi ili kuletamaendeleo kwa Taifa.

No comments